Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian |
Ufaransa
imetangaza kuwa itawatuma wanajeshi wake 300 kupambana na wapiganaji
wa makundi ya kiislam katika eneo kubwa la ukanda wa Sahel. Wakati
huu askari mmoja wa Ufaransa akiarifiwa kupoteza maisha kaskazini mwa
Mali.
akifahamisha
taarifa hii, waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian amesema
jukumu lao ni kuwafuata wanamgambo wa makundi ya kiislam
walikojificha katika maeneo ya kaskazini mwa Mali, Niger na Tchad na
sasa wanapanga kikosi cha wanajeshi mia tatu wataopelekwa katika
maeneo hayo.
Hata
hivyo waziri Ledrian amesema Ufaransa ilikuwa inalekea katika
mchakato wa kuhitimisha vita huko kaskazini mwa Mali, lakini askari
elfu moja watabaki katika eneo la Gao kaskazini mashariki mwa nchi
hiyo
Hayo
yanajiri wakati huu askari mmoja wa Ufaransa akiripotiwa kupoteza
maisha katika baada ya kukanyaga bomu la kutegwa ardhini lililotegwa
na wapiganaji wa makundi ya kiislam.
Viongozi
wa Ufransa kuanzia kwa rais francois Hollande wamezipeleka salam za
rambi rambi kwa familia ya mwanajeshi huyo na kusema kwamba amekufa
kishijaa wakati akipigania usalama wa dunia.
Ufanrasa
ilianzisha operesheni Serval Januari mwaka 2013 kuwasaidia wanajesi
wa Mali kupambana na makundi ya kiislam yaliokuwa yameteka miji ya
kaskazini na kuayasambaratisha.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire