Serikali
ya Marekani imemshawishi rais wa DRCongo Joseph Kabila Kabange
kuondoka madarakani ifikapo mwaka 2016 kama inavyoagiza katiba ya
nchi hiyo na imejikubalisha kutowa kitita kinachokadiriwa kufikia
dola za Marekani Milioni thalathini zai ziada katika kuunga mkono
mchakatoi wa uchaguzi nchini humo.
Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ambaye yu ziarani baranai
Afrika kwa lengo la kutatua mizozo iliokita mizizi katika mataifa ya
Afrika Hususan nchini Sudani Kusini na eneo la ukanda wa Maziwa makuu
amesema nchi yake inaimani kwamba katiba ya jamhuri ya kidemokrasia
ya Congo itaheshimiwa.
Wakati
huo huo mjumbe wa marekani katika Ukanda wa maziwa makuu Russell
Feingold ameweka wazi kwamba hawataki kuona rais Kabila anafanya
mabadiliko ya katiba au kuwania tena urais kwa muhula wa tatu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire