Rais wa
Ufaransa Francpis Hollande ameelekea nchini Ujerumani jioni hii
katika mji wa Rügen na Stralsund karibu na bahari ya Baltique
katika ngome ya Angela Merkel. Mzozo wa Ukraine, na siasa, Uchumi
ndio maswali yanayotarajiwa kugubikwa mazungumzo hayo.
Mualiko wa
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa rais wa Ufaransa Francois
Hollande katika eneo hilo la ufukwe wa bahari ya baltik ambako ni
ngome ya Merkel, ni ishara ya kudumisha uaminifu wa uhusiano wa
wakrito wa kidemokrasia na wa socialist baada kuaonekana kuwa mgumu
hapo mwanzoni.
Kansela
Merkel anapongeza hali ya maelewano ya ikulu ya Ufaransa na ahadi ya
jukumu la Manuel Valls hali ambayo utawala wa Ujerumani unaonakuwa ni
hatua nzuri na yenye mwelekeo sahihi.
Muungano
mpya wa kisiasa unaovikutanisha vyama vya Sociodemokrate na wa
liberali unaruhusu kupanua wigo wa kisiasa na kuonyesha nia ya
kushirikiana kuhusu swala la mzozo wa Ukraine. Paris na Berlin
wanaamini kwamba ni fursa nzuri ya kushirikiana kwa muda mrefu katika
swala la vikwazo dhidi ya Urusi.
Hakuna
kinachotarajiwa kuzungumziwa kuhusu kampuni ya Alstom, lakini
mawaziri wa Ujerumani wa Uchumi Arnaud Montebourg na Siegmar Gabriel
watakutana ili kuzungumzia swala hilo ambapo mfanyabiashar Siemens
ameonyesha nia ya kununuwa kampuni hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire