Kesi
ya Bingwa wa mbio za dunia za walemuavu Oscar Pistorius dhidi ya
mchumba wake Reeve Steenkamps imerudi tena kurindima leo, ambapo
mashahidi wawili waliokuwepo baada ya tukio hilo lililotokea Februri
mwaka 2013, wamesema Pistorius alivunjika nguvu baada ya kugunduwa
kuwa amemuuwa mpenzi wake.
Johan
Stander mmoja kati ya watu waliopigiwa sim na Pistorius, ameiambia
mahakama kwamba alipokea sim ya Pistorius majira ya saa tisa alfajiri
akimnasihi kuja kumsaidia kwani amempiga risase Reeve akihisi kuwa ni
jambazi.
Baada
ya kuwasili katika eneo la tukio akiwa na binti yake Carice Viljoen,
Johan Stander amesema walimkuta Pistorius akishuka ngazi huku akiwa
na mpenzi wake mikononi akiomba msaada wa kumpeleka mpenzi wake
Hospitalini huku machozi yakibubujika, akilia na kuonekana mwenye
huzuni kubwa.
Naye
binti wa Johan Stander alishindwa kuendelea kutowa ushahidi na
kujikuta akimwaga machozi na kueleza kwamba alihisi huenda Pistorius
atajipa sumu wakati alipokwenda kutafuta kitambulisho cha Reeve
ilikutambuwa wakati wa huduma ya kwanza.
Kinyuma
na ushaihidi mwingine, ambao unasema sauti ya mwanamke ambaye huenda
alikuwa Reeve akilalamika mbele ya muuaji, Carice Viljoen amesema
alisikia sauti ya ambayo anauhakika kwamba ni ya mwanaume.
Oscar
Pistorius mwenye umri wa miaka 27 anaweza kufungwa kifungo cha miaka
25 iwapo atakutwa na hatia ya kumuuwa mpenzi wake Reeve Steenkamp
mwanamitindo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire