Kiongozi
wa chama cha upinzani cha MSD nchini Burundi Alexis Sinduhije
amezuiliwa tangu jana asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Zaventem
mjini Brusels nchini Ubelgiji wakati alikua akitokea jijini Nairobi
nchini Kenya.
Viongozi
wa Burundi walitoa mwishoni mwa mwezi machi hati ya kukamatwa kwa
kiongozi huyo wa upinzani, akituhumiwa kuanzisha vuguvugu dhidi ya
utawala wa Pierre Nkurunziza.
Alexis
Sinduhije anatuhumiwa na serikali ya Bujumbura kwamba alihusika na
machafuko yaliyotokea mwezi machi kati ya wafuasi wake na polisi.
Taarifa
zaidi zinaarifu kwamba serikali ya Burundi kupitia ubalozi wake jiji
Brussels umewasilisha hati ya kukamatwa kwa mwanasiasa huyo. Jambo
ambalo serikali ya Ubelgiji inasema haiwezi kutekeleza amri ya
kurejeshwa kwa raia yeyote kwa sababu za kisiasa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire