Kiongozi
wa kundi la Boko Haram Aboubakar Shekau ameweka wazi mkanda wa video
unaowanyesha wasichana zaidi ya mia moja ambao wanashukiwa kuwa
wanafunzi waliotekwa hivi karibuni na kundi hilo kaskazini mwa
Nigeria na kuthibitisha kwa wote wamesilimu na kuwa waislam.
Katika
mkanda huo wenye dakika 27, Abubakar Shekau ameomba wafungwa wote
kutoka kundi la Boko Haram waachiwe huru kabla ya kuwaacha wasichana
hao ambao ametishia kuwaoza kwa bei kubwa, huku wasichana hao
wakionekana wote wamevaa hijabu na kuendelea kusoma Coran katika hali
tulivu.
Imekuwa
vigumu kujuwa eneo walipo wasichana hao. Jumla wasichana 276 ndio
wanaoshikiliwa na kundi hilo tangu April 14 huko Chibok katiks Jimbo
la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria ambako kunaeshi wa kristo
wengi. Polisi inasema wasichana 223 hawajulikani walipo.
Mkandao
huo wa video unawaonyesha takriban wasichana 130 waliovalia hijabu
nyeusi na yenye rangi ya kijivu, wakifunika nyuso zao wakikaa chini
eneo linalo fanana na msituni huku wakisoma Coran.
Hadi
sasa inekuwa vigumu kujuwa ni wapi walipo wasichana hao, licha ya
jumuiya ya kimataifa kutuma wataalam wa ujasusi kwa ajili ya kuwasaka
walipo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire