Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani Papa Francis ni miongoni mwa viongozi duniani waliungana na Nigeria katika kazi hii ya kutekwa kwa wasichana zaidi ya mia mbili
Rais
wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema kutekwa nyara kwa wasichana
zaidi ya mia mbili na kundi la kigaidi la Boko Haram majuma mawili
yaliyopita, itakuwa mwisho wa kundi hilo nchini humo.
Rais
Jonathan ameongeza kuwa jitihada zinazofanywa na Jumuiya ya Kimataifa
kuwaokoa wasichana hao walio mikononi mwa Boko Haram zitazaa matunda
na wanagmabo hao hawatakuwa pa kukimbilia.
Mataifa
ya Marekani, Uingereza, Ufaransa na China yanetuma watalaam wake
nchini humo kusaidia kuwaokoa wasichana hao wa shule ambao kundi hilo
linasema litawauza.
Rais
Jonathan amewashukuru wageni waliohudhuria mkutano wa Kimataifa wa
kiuchumi unaomalizika kesho jijini Abuja, kwa kile alichokisema ikiwa
hawangehudhuria kwa sababu ya uongo, wanagmabo hao wangejiona
washindi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire