Ni
mwaka wa pili tangu rais wa Ufaransa Francois Hollande alipochaguliwa
kuwa kiongozi wa nchi hiyo. Na tangu kukalia kiti cha Urais Francois Hollande amepoteza umaharufu mkubwa kufuatia kutotekeleza ahadi alizozitowa wakati akiomba kura kwa wananchi.
Rais
Hollande amewaambia Wafaransa kuwa licha ya uongozi wake wa miaka
miwili kukumbukwa na misukusuko ya hapa na pale, anafanya kila
kilicho ndano ya uwezo wake kulete mabadiliko yatakayoimarisha maisha
ya wananchi wa taifa hilo.
Kura
za maoni zinaonesha kuwa umaarufu wa kiongozi huo wa chama cha
Kisosolisti umepungua mno ikilinhganiswa na rais wa zamani Nicolas
Sarkozy aliyekuwa maarufu wakati kama huu wakati wa uongozi wake.
Rais
Hollande ameahidi kuimarisha uchumi wa taifa hilo na kuunda nafasi
zaidi za kazi wakati wa uongozi wake.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire