Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amefanya ziara ya kushtukiza
nchini Sudani Kusini ili kulazimisha pande mbili zinazo zozana nchini
humo kusitisha mapigano katika nchi hiyo inayo kabiliwa na kitisho
cha njaa na kutokea kwa mauaji ya kimbari.
Hizi
ni juhudi za hali ya juu za kidiplomasia kujaribu kuzishwawishi pande
mbili husika na mzozo huo angalau kusitisha mapigano yalioanza
kushuhudiwa Desemba 15 mwaka jana katika taifa hilo changa kuliko
yote barani Afrika.
Baada
ya kukutana na rais salva Kiir, hatimyae amekubali kukutana ana kwa
ana na mpinzani wake Riek Machar kiongozi wa waasi walioiteka miji
kadhaa yenye utajiri wa mafuta.
John
Kerry amewataka waasi na wanajeshi wa serikali kuheshimu makubaliano
ya kusitishwa vita yaliofikiwa Januari mwaka huu na ambayo hayajawahi
kuheshimiwa na kuacha kuwashambulia raia wasiokuwa na hatia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire