Rais
wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi ambaye pia alikuwa
makamu wa rais Riek Machar wanakutana kwa mara ya kwanza ana kwa ana
jijini Addis Ababa Ethiopia, kujaribu kupata mwafaka wa kumaliza
machafuko yanayoendelea katika taifa lao kwa miezi mitano sasa.
Kukutana kwa viongozi hawa chini ya wasuluhishi wa mgogoro huo kutoka
Mataifa ya Afrika Mashariki IGAD wakiongozwa na Waziri Mkuu wa
Ethiopia Hailemariam Desalegn kumewapa wananchi wa Sudan Kusini
matumaini ya kurejea kwa usalama katika taifa lao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire