Viongozi
wa kanda ya Afrika Mashariki wamekutana jijini Nairobi nchini Kenya
Ijumaa hii na kuzindua mfumo wa pamoja wa Kieletroniki kurahihisha
usafirishaji wa bidhaa na kufanya biashara baina ya Mataifa hayo.
Hii
inaamanisha kuwa wafanyibiashara kutoka mataifa ya Kenya, Uganda,
Tanzania , Rwanda, Burundi na Sudan Kusini wataweza kuwasilisha
nyaraka zao ikiwemo vibali vya kufanya biashara,malipo mbali,bali
katika eneo moja kwa njia ya eletroniki.
Akizindua
mfumo huo rais wa Rwanda Paul Kagame, amesema mfumo huu utaiharakisha
biashara na shirikish la Afrika Mashariki.
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta naye amesema mfumo huu ikia utatekelezwa
ipasavyo, ndoto ya shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki
litatimia.
Tanzania
iliwakilishwa katika mkutano huo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, huku
Burundi ikiwalishwa na Makamu wa pili wa rais Gervais
Rufyikiri.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire