Ikiwa
leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na maradhi ya saratani, shirika
la afya duniani WHO, linasema kuwa jumuiya ya kimataifa inayo nafasi
na uwezo mkubwa wa kudhibiti maradhi ya saratani ambayo sasa
yameongezeka kwa kasi kwenye nchi zinazoendelea.
Huu
ndio ujumbe unaotolewa hii leo na shirika la afya duniani wakati wa
maadhimisho ya siku ya saratani duniani ambayo huadhimishwa tarehe 4
ya kila mwaka, ambapo kwa mujibu wa takwimu za shirika hili, asilimia
70 ambayo ni sawa na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 8, hufariki
kila mwaka duniani kutokana na maradhi haya na hasa kwenye nchi
zinazoendelea.
WHO
inasema kuwa iwapo hatua hazitachukuliwa mapema kudhibiti maradhi
haya, idadi itaongezeka kutoka watu milioni 7 na laki 6 mwaka huu
hadi kufikia watu milioni 9 kwa mwaka 2030.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire