Mahakama
moja nchini Misri imethibitisha hukumu ya adhabu ya kifo kwa zaidi ya
raia 183 waliopatikana na hatia ya mauaji ya polisi 13 jirani na mji
wa Cairo August mwaka 2013.
Hukumu
hii inafuatia uamuzi wa mahakama hiyo iliyoufanya mwezi December
mwaka jana ambapo iliwakuta na hatia zaidi ya raia 188 kwa tuhuma za
mauaji ya polisi, ambapo kwenye hukumu ya hii leo, mahakama hiyo
imewaachia huru watuhumiwa wawili huku mwingine akihukumiwa adhabu ya
kifungo cha miaka 10 jela.
Kufutiwa
mashtaka kwa watuhumiwa hawa wawili kumekuja baada ya mahakama
kubaini kuwa watuhumiwa hao wamefariki, ambapo kuthibitishwa kwa
hukumu hii kumetokana na uamuzi wa mufti mkuu wa nchi hiyo
kukubaliana na uamuzi wa awali wa mahakama.
Watuhumiwa
hawa ambao 143 kati yao walikuwa wanashikiliwa na polisi,
walipatikana na hatia ya kuhusika na vurugu za mwezi August mwaka
2013 ambapo wanadaiwa kuwa walivamia kituo cha polisi cha Kerdassa na
kuua askari 13 wa kituo hicho.
Toka
kuangushwa madarakani kwa utawala wa Mohamed Morsi mwezi July mwaka
2013, watu wanaokadiriwa kufikia elfu 1 na 400 wameuawa na polisi
wakati wa maandamano.
Mashirika
ya kutetea haki za binadamu yameelezwa kuguswa na hukumu hizi ambazo
zimekuwa zikitolewa na mahakama yakidai kuwa nyingine zimechochewa
kisiasa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire