Pages

mercredi 4 février 2015

KENETH KAUNDA KINARA WA UHURU WA ZAMBIA ALAZWA HOSPITALINI


Rais wa zamani wa Zambia kinara wa uhuru wa taifa hilo Keneth Kaunda mwenye umri wa miaka 90 sasa, amelazwa tena Hospitalini jijinin Lusaka hii leo jumanne.

Taarifa hii imethibitishwa na binti yake Cheswa Silwizya ambae amesema kwamba hali ya baba yake ni nzuri na anaelekea kupona na kujiuzuia kutowa sababu za kulazwa tena Hospitalini na kusema kwamba ma daktari pekee ndio wanaofaham
Kinara huyo wa uhuri wa Zambia alilazwa pia Hospitalini mwaka jana kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni mchoko.

Keneth Kaunda aliongoza Zambia kwa takriban miaka 27 tangu kupatikana kwa uhuru wa taifa hilo mwaka 1964 na alikuwa miongoni mwa vinara wakuu watetezi wa uhuru barani Afrika na aliwapokea viongozi wengi watetezi wa Uhutu katika nchi mbalimbali hususan kinara wa chama cha ANC Nilson Mandela

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...