












Bob Rugurika alitiwa nguvuni mwezi uliopita akituhumiwa kuhusika katika mauaji ya watawa watatu vikongwe raia wa Italia, waliouawa katika mauaji ya kutatanisha.
Mashirika ya kiraia, viongozi mbalimbali nchini humo wametowa wito kwa serikali kuunda tume huru itayo endesha uchunguzi wa kina kuhusu mauaji hayo, badala ya kumuweka korokoroni mwanahabari huyo.
Kutiwa nguvuni kwa mkurugenzi wa RPA kulitokana na kituo chake kupeperusha sauti ya mtu aliedaikuwa yeye ndie aliehusika na mauaji hayo na kuwataja viongozi kadhaa wa serikali kuwa ndio walioyapanga, na kwamba wao walikuwa tu watekelezaji.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire