Katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, juma hili amewatuhumu viongozi
wanaohasimiana nchini Sudan Kusini, akidai kuwa wameweka mbele
maslahi yao kuliko maslahi ya wananchi ambao waliwachagua na kuwaweka
madarakani.
Kauli
ya Ban anaitoa wakati huu ambapo rais Salva Kiir na mwenzake Dr Riek
Machar wakishindwa kuafikiana kuhusu namna ya kugawana madaraka ili
kumaliza mzozo wa kisiasa uliosababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe
nchini humo.
Kwenye
taarifa yake, katibu mkuu Ban ameelezwa kusikitishwa na namna
viongozi hao wanavyoshindwa kufikia suluhu ya kisiasa licha ya mara
kadhaa kutiliana saini makubaliano ya kusitisha vita, ambapo
ameongeza kuwa suluhu ya weza patikana nchini humo iwapo viongozi
hawa wataweka mbele maslahi ya taifa na wananchi wao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire