Jeshi
la Uganda limefahamisha kwamba litafanya uchunguzi kupitia vinasaba
vya mwili wa mtu aliezikwa hivi karibuni kubaini iwapo ni kiongozi
numba mbili wa kundi la waasi wa Lord Resistence Army LRA anedaiwa
kuawa mwaka mmoja uliopita.
Kwa
mujibu wa msemaji wa jeshi la Uganda Paddy Ankunda viongozi wa Uganda
wanahisi kuwa wamelipata kaburi alipozikwa Okt Odhiambo mtu wa karibu
sana na kiongozi wa LRA Joseph Kony.
Pandi
akunda amesema tayari vinasaba hivyo wamevipata, na sasa wanafanya
uchunguzi wa DNA ili kubaini iwapo kweli ni kiongozi huyo. Hata hivyo
msemaji huyo wa majeshi ya Uganda amaketaa kusema ni eneo gani
walipogundua kaburi hilo linalo sadikiwa ndiko alikozikwa mmoja kati
ya viongozi wa kundi la RLA.
Uganda
na Marekani zilibaini mwezi Februari mwaka jana uwezekanao wa kutokea
kwa kifo cha Odhiambo ambae alikuw amiongoni mwa wanaotafutwa na
mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC kutokana na vitendo vya ujunjifu
wa haki za binadamu vinavyotekelezwa na wapiganaji wa kundi hilo.
Iwapo itathitishwa kifo cha kiongozi huyo, basi Joseph Kony atakuwa
ni kiongozi pekee wa kundi hilo ambae bado anatafutwa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire