Serikali
ya Niger inajiandaa kutuma wanajeshi wake kupigana sambamba na
majeshi ya nchi jirani dhidi ya kundi la kiislamu la Boko Haram saa
chache baada ya mamia ya watu kuuawa kwenye mashambulizi
yaliyotekelezwa na wapiganaji hao kwenye mpaka wa nchi ya Niger na
Nigeria.
Kuingilia
kati kwa majeshi ya Niger kwenye vita dhidi ya kundi la Boko Haram,
kutaongeza nguvu ya majeshi mengine ya nchi jirani kutokea kaskazini
mwa nchi hiyo katika kukabiliana na wapiganaji hao ambao katikati ya
wiki hii waliwaua wanajeshi 19 kwenye mpaka na nchi ya Cameroon mjini
Gambori.
Mashambulizi
ya kundi la Boko Harama yametekelezwa saa chache baada ya majeshi ya
Chad kuingia kwenye mstari wa mbele wa mapambano na kufanikiwa
kuuchukua mji wa Gambori na kutangaza kuwauwa zaidi ya wapiganaji 200
wa kundi la Boko Haram.
Kwa
mujibu wa msemaji wa Serikali ya Niger, bunge la nchi hiyo
linatarajiwa kuketi siku ya Jumatatu kupiga kura kupitisha mpango wa
Serikali kutuma wanajeshi wake kuungana na vikosi vya Cameroon, Chad
na Nigeria kuwakabili wapiganaji wa kundi hilo.
Zaidi
ya raia elfu 3 wameuawa toka kundi hilo lilipoanza uasi mwaka 2009,
huku wengine nusu milioni wakilazimika kuwa wakimbizi ndani ya nchi
yao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire