Machafuko
ya kivita yanayo likumba taifa la Sudani Kusini kwa kipindi cha mwaka
mmoja yamesababisha mamia ya watu kupoteza maisha bila shaka hususan
katika eneo la kaskazini mwa nchi. Naibu mkuu wa tume ya haki za
binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Ivan Simonovic mabae hivi karibuni
amezuru nchini humo, amesema ni vigumu kujuwa takwimu sahihi lakini
wanakadiria kuwa mamia na ma elfu ya watu wameuawa.
Kulingana
na kiongozi huyo, eneo la Kaskazini ndilo lililoathirika zaidi na
vita hivyo baada ya mara kadhaa kushuhudia makabiliano hususan katika
miji ya Bentui na malakal eneo la Kaskazini pamoja na Joglei na
jimbo la unity kaskazini na Hight Nil, kaskazini mashariki.
Hayo
yanajiri wakati huu Umoja wa Mataifa ukitowa wito kwa jumuiya ya
kimataifa wa kukusanya dola bilioni 1.8 sawa na Euro 1.5, kwa ajili
ya msaada wa wananchi wa Sudani Kusini wanaokabiliwa na baa la njaa
baada ya machafuko ya miezi 13 ya wenyewe kwa wenyewe.
Mkuu
wa operesheni ya misaada kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos ambae
hivi karibuni alikuwa nchini Sudani Kusini amesema hali ni tete, na
kwamba mapigano lazima yakomeshwe.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire