Watu zaidi ya 20 wameuawa nje kidogo ya mji wa Beni
mashariki mwa jamhuri ya kjidemokrasia ya congo, baada ya kundi la
watu wasiojulikana kukivamia kijiji cha Mayangos usiku wa kuamkia leo
siku ya jumatano. Maafisa wa polisi wamebainisha.
Wakuu
wa serikali pamoja na maafisa wa jeshi la umoja wa mataifa, Monusco
wanasema waasi wa Uganda kutoka kundi la ADF Nalu ndio wametekeleza
mauaji hayo.
Mauaji
haya yanafanyika siku chache baada ya jeshi la serikali ya DRC, FARDC
kutangaza kuwa limeanza mpango wa kupambana na waasi wa kihutu toka
Rwanda wa FDLR, mashariki mwa nchi hiyo.
Tangu
mwezi oktoba hadi desemba mwaka wa jana watu mia mbili na sitini
waliuawa katika maeneo hayo ya Beni, wengi wakikatwa kwa mapanga,
majambia, na visu, hali kadhalika kwa silaha; huku vikosi vya jeshi
la serikali vikielezea kuwa juhudi za kutokomeza waasi zinaendelea.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire