Waziri
wa mbo ya ndani nchini Burundi Edouard Nduwinama ametahadharisha hii
leo kuhusu tukio lolote la kuzua vurugu nchini humo siku moja baada
ya kushuhdiwa maandamano makubwa ya kumuunga mkono muandishi wa
habari, na kuutuhumu upinzani kwamba unafanya kila mbimnu kuvuruga
mchakato wa uchaguzi.
Hakuna
takwimu kamili zilizotolewa lakini muandishi wa habari wa AFP
aliekuwepo jijini Bujumbura aleza kwamba maelfu kwa ma mia ya watu
walimiminika jana katika barabara mbalimbali za jiji kumpokea
mkurugenzi wa kituo cha radio RPA ambae alikuwa ameachiwa huru kutoka
katika jela kuu la Muramvya kwenye umbali wa kilometa zaidi ya 50 na
Bujumbura.
Waziri
Nduwimana amesema wanafuatilia tangu kipindi kadhaa wito unaotolewa
na upinzani wa kuwataka watu kuandamana na kwamba kilicho shuhudiwa
jana ilikuwa ni kipimo kwa hawa na wale kuangalia uwezekanao wa
kutekeleza mpango wao.
Hata
hivyo waziri Nduwimana amekiri kwamba katiba ya burundi inaruhusu
watu kuandamana, lakini kilichofanyika jana amesisitiza ni uasi
ulioandaliwa.
Lengo
hasa la kuandaa maandamano waziri huyo wa mambo ya ndani amesema
radio RPA na washirika wake wa upinzani wanalenga kuangusha taasisi
za serikali na kuzuia uwepo wa uchaguzi mkuu wa rais nchini humo, na
kwamba serikali haitokubali tena jambo hilo kutokea.
Wizara
ya mambo ya ndani ilikuwa imekataza kufanyika kwa maandamano, lakini
wananchi walitupilia mbali katazo la serikali na kuandamana kwa
kishindo huku polisi wakiwaacha wananchi ambao waliandamana kwa
utilivu, kabkla ya polisi kuinglia kati dakika za mwisho kwa
kuwatawanya kwa kuwamwagia maji.
Joto
la kisiasa limeendelea kupanda nchini Burundi wakati huu nchi hiyo
ikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais Juni ijayo, hasa kuhusu hatuwa
inayosubiriwa ya kujichagulisha kwa muhula wa 3 au la kwa rais wa
nchi ihyo bwana Pierre Nkurunziza.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire