Serikali
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC imesema kuwa imekataa ombi
la tume ya Umoja wa mataifa nchini humo kushirikiana na jeshi lake
katika operesheni ya kuwasambaratisha wapiganaji wa kundi la FDLR, na
kutoa onyo dhidi ya taasisi za kimataifa kuingilia masuala yake ya
ndani.
Juma
lililopita, tume ya Umoja wa Mataifa ilitangaza kujiondoa katika
operesheni ya pamoja na jeshi la Serikali ya DRC, kushiriki
operesheni maalumu ya kuwasaka waasi wa Rwanda wa FDLR kwa kile umoja
wa mataifa unataka kwanza majenerali wawili wa juu wa jeshi la DRC
wafutwe kazi kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya ukiukwaji wa haki
za binadamu.
Waziri
wa habari na msemaji wa serikali ya DRC, Lambert Mende, amesema
serikali yake inakataa rasmi ombi la Umoja wa mataifa na kwamba
wanajeshi hao hawatafutwa kazi kwa shinikizo na kuzionya taasisi za
Umoja huo kutoingilia masuala yake ya ndani.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire