Polisi
nchini Ufaransa, inawashikilia watu 8 wanaotuhumiwa kujihusisha na
mtandao wa kusafirisha vijana kwenda nchini Syria na Iraq kupigana
vita sambamba na makundi ya kiislamu, wizara ya mambo ya ndani nchini
humo imethibitisha.
Waziri
wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve amewaambia waandishi
wa habari kuwa watu hao wamekamatwa kutoka kwenye maeneo mbalimbali
ya jiji la Paris na kusini mwa mji wa Lyon.
Kukamatwa
kwa watu hawa kumekuja ikiwa imepita wiki moja tu, toka polisi nchini
humo watangaze kuwakamata watu 5 kwenye mji mdogo wa Lunel kusini mwa
nchi hiyo, eneo ambalo vijana wengine 20 wanadaiwa walisafiri kwenda
nchini Syria.
Mwezi
mmoja uliopita kwenye hotuba yake, waziri mkuu Manuel Valls alisema
kuwa vijana kati ya 1400 ambao wanaishi Ufaransa wamejiunga ama
walikuwa wamepanga kujiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislamu
nchini Syria na Iraq.
Nchi
ya Ufaransa hivi karibuni imefanya msako maalumu uliolenga kuwakamata
watu wenye uhusiano na makundi ya kiislamu, hatua inayokuja baada ya
mwezi mmoja uliopita vijana wawili kutekeleza shambulio jijini Paris
na kuua watu 17.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire