Askari
mmoja wa Burundi aliepo kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha
kulinda amani Minusca, ameuawa juzi jumapili na askari mwenzake,
taarifa ya Munusca imethibitisha hapo jana.
Taarifa
hiyo imesema askari huyo wa Burundi katika kikosi cha kimataifa cha
kulinda amani ameuawa jumapili Februari 8 mwaka 2015 jijini Bangui
baada ya kupigwa risase na mwenzie ambae ametiwa ngubuni mara moja.
Minusca
imeagiza uchunguzi ufanyike mara moja ili ukweli ufahamike kuhusu
tukio hilo.
Huyu
ni mwanajeshi wa nne kupoteza maisha tangu kuanzishwa kwa vikoso
hivyo septemba 15 mwaka 2014 kutoka jeshi la Umoja wa Afrika Misca.
Tangu
kuangushwa kwa utawala wa rais Francois Bozize mwezi March 2013 na
muungano wa waasi wa Seleka ambao walishinikizwa kuachia madaraka,
nchi hiyo imeshuhudia machafuko ya kisiasa yasiokuwa na mfano ambapo
kundi la waasi wa kikristo la Anti Balaka na waasi wa seleka ambao
wengi wao ni waislam.
Uwepo
wa aina 3 za vikosi vya Kimataifa, ikiwa ni pamoja na kikosi cha
Ufaransa Sangaris, kikosi cha Umoja wa Ulaya Eufor pamoja na Minusma,
umesababisha kurejesha utulivu bila hata hivyo kufaanikiwa
kuliunganisha taifa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire