Watu
22 wameripotiwa kufa mpaka muda huu baada ya ndege ya abiria
inayomilikiwa na shirika la TransAsia ya nchini Taiwani kuanguka
kwenye mto mmoja mjini Taipei ikiwa na watu 58, hii ikiwa ni ajali ya
pili katika kipindi cha miezi 7.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa ndege hiyo aina ya
ATR 72-600, ilionekana kupoteza uelekea na kukosakosa baadhi ya
majengo yaliyokuwa jirani na daraja linalopitisha maji ya mto Taipei.
Polisi
wanasema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kuopoa miili ya watu 22 na
wengine wakiwa hai huku zoezi la kuokoa watu zaidi likiendelea wakati
huu ambapo wataalamu wa masuala ya ndege wakiwa wamefanikiwa kupata
visanduku vya sauti vya ndege hiyo.
Awali
baadhi ya vituo vya redio na televisheni vilionesha na kurusha
matangazo ya sauti walizodai ni kutoka kwenye kisanduku cha sauti cha
ndege hiyo, ambapo marubani wa ndege hiyo walisikika wakiomba msaada
wa dharura baada ya moja ya injini zake kuwaka moto.
Hata
hivyo polisi wamekanusha taarifa hizo wakidai kuwa licha ya kuvipata
visanduku vya sauti, hawajaanza uchunguzi wala kufanikiwa kusikiliza
mawasiliano ya mwisho ya marubani hao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire