Ikiwa
ni takriban majuma mawili yamesalia kabla ya wananchi wa Nigeria
hawajapiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa rais, chama tawala nchini
humo kinakabiliwa na mtihani mwingine wa kisiasa baada ya viongozi
kadhaa wa makanisa nchini humo kuonesha kumuunga mkono kiongozi wa
upinzani.
Wakati
wachambuzi wa mambo wakiendelea kumpa nafasi rais Goodluck Jonathan
kuibuka na ushindi kwenye uchaguzi wa February 14 mwaka huu,
wataalamu wanadai kuwa kuna mambo mawili ambayo yanaweza kukiondoa
chama tawala cha Peoples Democratic madarakani.
Wataalamu
hao wanasema kuwa cha kwanza ni uungwaji mkono wa kiongozi wa
upinzani Muhamadu Buhari na waumini wa dini ya kikristo kusini mwa
nchi hiyo, na kutoungwa mkono kwa rais Jonathan katika maeneo yenye
waumini wengi wa Kiislamu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire