Mtoto
mmoja kichanga amepoteza maisha nchini Canada huku ndugu zake wengine
wanne wenye umri kati ya miaka 2 na 7 wakiwa katika hali mahtuti
baada ya mama yao kupulizia dawa ya kuuwa wadudu ndani ya nyumba,
dawa ambayo inadaiwa kuwemo sumu.
Duru
kutoka kwa mmoja wa familia hiyo ameeleza kwamba mama huyo alitumia
dawa hiyo kutoka nchini Pakistan ili kuuwa wadudu waliokuwa
wameshambulia nyumba hiyo, bila hata hivyo kujuwa kwamba inasumu
ndani yake.
Habari
zaidi zinaeleza kuwa dawa hiyo hutumiwa katika sekta ya kilimo kwa
ajili ya kulinda mbolea katika ghala baada ya kukaa kwa muda mrefu.
Mtoto huyo mchanga alifariki muda mfupi tu baada ya kufikishwa
hospitalini.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire