Pages

mercredi 11 février 2015

MONUSCO YATANGAZA KUSITISHA MSAADA WAKE WA KIJESHI KATIKA OPERESHENI YA FDLR


Umoja wa Mataifa umetangaza kusimamishwa utoaji wa msaada kwa jeshi la jamahuri ya kidemokrasia ya Congo katika opersheni yake dhidi ya kundi la waasi wa kihutu wa Rwanda waliopiga kambi mashariki mwa nchi hiyo wa FDLR.

Afisa mmoja wa Umoja wa mataifa ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP uamuzi huu kutokana na utata uliojitokeza hivi karibu kufwatia uteuzi wa majenerali wawili wanaotuhumiwa kwa makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu kuongoza operesheni ya kuwasaka waasi hao.

Awali, Ujumbe wa Umja wa mataifa nchini DRC - MONUSCO umeipa serikali ya Kinshasa makataa hadi tarehe 13 Februari kutengua uteuzi wa majenerali Bruno Mandevu na Sikabwe Fall, jambo ambalo serikali hiyo imetupilia mbali na kukanusha tuhuma zinazowakibili wahusika hao.

Hata hivyo, afisa huyo amebaini kuwa pamoja na uamuzi huo, MONUSCO itaendelea kutoa msaada wake katika shughuli nyingine za kijeshi kwa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC na kwamba bado mazungumzo ya ngazi za juu yanaendelea ili kufikia mwafaka.

Bruno Mandevu na Sikabwe Fall wameorodheshwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO kwenye orodha ya maafisa wa jeshi la Congo ambao wanadaiwa kushiriki katika kutekeleza vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...