Baada
ya miezi 13 ya mapigano na mara saba ya kutiliana saini mikataba ya
kusitisha mapigano bila mafanikio, wanadiplomasia wa kimataifa
wanaona kuwa kwasasa mkataba wowote wa amani utakaokubaliwa na
viongozi wanaohasimiana nchini Sudan Kusini utakuwa bora katika
kusaidia kutuliza mzozo wa nchi hiyo.
Kwa
mujibu wa makubaliano ya hivi karibuni yaliyopendekezwa na viongozi
wa nchi za IGAD mwishoni mwa juma mjini Addis Ababa, yatashuhudia
rais Salva Kiir akisalia kuwa rais huku Dr Riek Machar akirejeshwa
kwenye nafasi yake ya makamu wa rais nafasi aliyoishikilia mpaka
mwezi July 2013 ambapo alikimbia.
Riek
Machar na rais Salva Kiir Jumapili hii walikubaliana kutiliana saini
mkataba wa kusitisha mapigano lakini wakashindwa kukubaliana namna ya
kugawana madaraka kujaribu kumaliza mzozo wa kisiasa unaofukuta
nchini humo.
Makubaliano
haya yanajiri ikiwa yamepita majuma kadhaa toka watiliane saini
makubaliano ya kuunganisha tena chama tawala cha SPLM, makubaliano
yaliyosimamiwa na Chama tawala nchini Tanzania CCM
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire