Mashirika
ya kiraia nchini Burundi juma hili yametoa wito kwa rais Pierre
Nkurunzinza anayedaiwa kutaka kuongeza muda ili kumpa nafasi ya
kuwania muhula mwingine watatu kwenye uchaguzi wa mwezi June mwaka
huu, kuachana na mpango wake ili kuepusha vurugu zinazoweza
kujitokeza.
Majuma
mawili yaliyopita muungano wa mashirika ya kiraia zaidi ya 304 nchini
Burundi yalizindua kampeni maalumu kupinga rais Nkurunzinza kuwania
muhula mwingine wa tatu, ambapo waliandika barua ya siri kwa rais
February 4 mwaka huu kumuomba asigombee tena kwenye uchaguzi ujao.
Viongozi
wa mashirika hayo wanasema kuwa kutokana na kutojibiwa kwa barua yao,
wataendelea kupiga kelele na kuwashawishi wananchi kutounga mkono
uamuzi wowote wa Serikali utakaompa nafasi rais Nkurunzinza kuwania
muhula wa tatu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire