Licha
ya makubaliano ya hivi karibuni kati ya viongozi wawili mahasimu wa
Sudan Kusini, Serikali ya Marekani kupitia waziri wake wa mambo ya
kigeni John Kerry, ametaka baraza la usalama la umoja wa mataifa
kupitisha azimio la kuiwekea vikwazo vya kununua na kuuziwa silaha
kwa nchi ya Sudan Kusini.
Licha
ya mijadala inayofanyika mara kwa mara kwenye baraza la usalama la
Umoja wa mataifa kutaka nchi hiyo kuwekewa vikwazo, kumekuwa na
kusuasua kufikiwa kwa maazimio ya pamoja kuhusu hatua za kuchukua
dhidi ya rais Salva Kiir na mwenzake Dr Riek Machar.
Hivi
sasa Serikali ya Marekani inataka kupitishwa kwa azimio maalumu
kuhusu nchi ya Sudan Kusini na kwamba viongozi wake ni lazima
wawekewe vikwazo kushinikiza kufikiwa kwa suluhu nchini humo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire