Wanajeshi
wa nchi ya Sudan wanatuhumiwa kuwabaka wanawake na wasichana zaidi ya
mia mbili katika jimbo la Darfur mwaka uliopita, ikiwa ni tukio baya
zaidi kuripotiwa na kwamba uchunguzi lazima ufanyike dhidi ya vitendo
vya uhalifu wa kibinadamu, shirika la Human Right Watch limesema.
Katika
ripoti yake yenye kurasa 48, Human Right Watch imeeleza kuguswa na
namna ambavyo vikosi vya Serikali vimeshiriki katika kutekeleza
uhalifu huu licha ya mara kadhaa utawala wa Khartoum kukanusha
wanajeshi wake kuhusika kwenye tukio hilo la Mwezi October mwaka jana
mjini Tabit.
Ripoti
hiyo inasema kuwa wanajeshi walikuwa wakipita nyumba kwa nyumba
wakipora mali, kuwapiga wakaazi, kuwakamata wanaume ambao
walichukuliwa huku wanawake na wasichana wakibakwa kwenye nyumba zao,
ripoti hii imeonesha.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire