Kesi
ya kumiliki danguro na kunua wasichana wa umri mdogo kushiriki nao
kimapenzi dhidi ya mkuu wa zamani wa shirika la fedha duniani IMF,
Dominique Strauss-Kahn imeanza kusikilizwa tena hii leo kwenye
mahakama moja mjini Lille.
Strauss-Kahn,
mchumi mwenye umri wa miaka 65 hivi sasa amepandishwa kizimbani
kwenye mahakama ya jiji la Lille akituhumiwa kuwa kiini cha kundi la
watu wenye fedha wanaonunua wasichana kwaajili ya kuwatumia kwenye
sherehe zao mjini Brussels, Paris na Washington.
Kesi
hii inayotarajiwa kudumu kwa majuma matatu, itashuhudia kiongozi huyu
ambaye wakati fulani alitajwa kuwa kinara wa mbio za urais nchini
Ufaransa, akisimama kizimbani sambamba na mameneja wa hoteli, polisi,
freemasons pamoja na kaka yake anayefahamika kwa jina la Dodo the
Pimp.
Wachambuzi
wa mambo wanasema kuwa iwapo Dominique Strauss-Kahn atapatikana na
hatia ya makosa yanayomkabili huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10
au kulipa faini inayokadiriwa kufikia dola za Marekani milioni 1 na
laki 7.
Awali
mwendesha mashtaka kwenye kesi hii alitaka kufutwa kwa kesi hiyo kwa
kile alichodai kukosekana kwa ushahidi wa kutosha dhidi yake, ombo
ambalo hata hivyo mahakama ililikataa na kuagiza kesi hiyo kuendelea.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire