Baraza
la usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kuachiwa huru mara moja kwa
mateka anayeshikiliwa na wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Islamic
State, wakati huu utawala wa Jordan ukiapa kufanya kila
linalowezekana kuhakikisha raia wake anaachiwa na kundi hilo.
Juma
hili baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mauaji ya raia
mwingine wa Japan Kenji Goto na kukiita kitendo hicho cha kinyama
huku kundi hilo likiapa kumuua ribani raia wa Jordan wanaemshikilia
mateka.
Haya
yanajiri ambapo mwishoni mwa juma serikali ya Jordan kupitia msemaji
wake, Mohammad al Moman amesema Serikali yao iko tayari kubadilishana
wafungwa na kundi hilo lakini kwanza wanataka hakikisho kuwa raia wao
yuko hai.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire