Baraza
la Senet nchini Burundi, limeidhinisha majina ya viongozi wa idara ya
upelelezi yaliowasilishwa na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ikiwa
ni miezi kadhaa kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais.
Rais
Nkurunziza amemteuwa Brigadia jenerali Etienne Ntakarutimana
anaelezwa kuwa mtu muaminifu kwake na ambae ameidhinishwa na barazala
Seneti bila pengamizi baada ya kuchaguliwa na wajumbe 37 dhidi ya 37
waliokuwepo bungeni.
Jenerali
Ntakarutimana mwenye umri wa miaka 43 ni mionogni mwa viongozi wa
kundi la waasi zamani wa CNDD-FDD lililoongozwa na rais Nkurunziza
ambalo liligeuka kuwa chama madarakani kwa sasa, aliwahi kuongoza
idara ya ujasusi katika jeshi la Burundi.
Mtangulizi
wake aliekalia nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu, brigadia
jenerali Godefroid Niyombare pamoja na mkuu wa itifaki kwenye idara
hiyo walifutwa kazi pamoja na mkuu wa usalama wa ndani. Kisa na mkasa
chaelezwa ni baada ya viongozi hao kumshauri rais Nkurunziza
kutowania muhula mwingine watatu katika uchaguzi mkuu wa Juni.
Kwa
sasa inaelezwa kwamba rais Nkurunziza amemteuwa mtu muaminifu kwake
ambae atakuwa na kibarua kigumu cha kusimamia usalama wakati rais
Nkurunziza atapotangaza kuwania urais kwa muhula wa 3 na kukabiliana
na matukio yatayo tokana na hatuwa hiyo, hususan maandamano.
Rais
Nkurunziza hajatangaza rasmi kuwania muhula wa 3, lakini kumekuwa na
dalili tosha zinazoonyesha kwamba anania ya kugobmea kwa mara ya 3,
jambo ambalo lipo kinyume na katiba ya nchi hiyo.
Mbali
na upinzani nchini humo unaopinga hatuwa hiyo ya kuwania muhula wa 3,
rais Pierre Nkurunziza anakabiliwa pia na upinzani wa ndani katika
chama chake, ambapo wapo viongozi ambao wamemtaka atowe nafasi kwa
mtu mwingine.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire