Oscar
Pistorius mwanariadha mlemavu kutoka nchini Afrika Kusini
anayetuhumiwa kumuua mpenzi wake kwa kumpiga risasi mwaka uliopita,
amelazimika kuuza nyumba yake aliikomuulia mpenzi wake ili kuwalipa
mawakili wake.
Imebainika kuwa Pistorious ameuza nyumba yake Dola
laki nne na elfu themanini, ili kuweza a kuwalipa mawakili wake dola
elfu tisa kila siku.
Kesi
dhidi yake imekuwa ikiendelea kwa wiki kadhaa sasa na amekanusha
kumuua mpenzi wake Reeva Stenkamp kwa makusudi. Tangu kuanza kwa kesi
hii, Pistorius hajajihusisha na shughuli za zaidi ambazo zilikuwa
zinampa kipato cha Dola laki tano kila mwaka.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire