Nchini
Afrika Kusini, chama tawala cha ANC kinaongoza wakati huu kura
zikiendelea kuhesabiwa baada ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu hapo
jana.
Matokeo ya
hivi punde yanaonesha kuwa chama cha ANC kinaongoza kwa asilimia
sitini , huku kile cha Democratic Aliance kikiwa na asilimia 22
wakati chama cha aliyekuwa kiongozi wa vijana katika chama cha ANC
Julius Malema cha Economic Freedom Fighters, kikiwa cha tatu.
Ilikuwa
imetabiriwa kuwa licha ya viongozi wa chama cha ANC kukumbukwa na
kashhfa za ufisadi kitapata ushindi na kile cha Democratic Alliance
kitaongeza viti vyake bungeni.
Baada ya
wabunge 400 kuchaguliwa watakuwa na jukumu la kumchagua rais wa nchi
hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire