wakati
rais wa Nigeria Goodluck Jonhattan akitowa wito kwa serikali ya
Marekani na mataifa mengine kumsaidia kutatua hali ya usalama nchini
Mwake, kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakr Shekau ametowa mkanda
wa Video ambao anajigamba kuwa kundi lake ndilo lililohusika na
utekaji nyara wa wasichana 220 katika wiki mbili zilizopita.
Hayo
yanajiri wakati huu hasira ikipanda miongoni mwa wananchi wa Nigeria
wakiilaumu serikali ya nchi yako kutofanya lolote katika juhudi za
kuwatafuta watoto hao waliotekwa nyara tangu April 14.
Rais
Goodluck ameahidi kuzidisha juhudi za kuwatafuta wasichana hao wakati
huu kukiandaliwa mkutano wa kimataifa jijini Lagos chini ya Ulinzi
mkali baada ya kutokea mashambulio mawili mjini hapo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire