Mkurugenzi
mkuu wa mbuga la wanyama ya Virunga mashariki mwa DRCongo
Emmanuel de Mérode anaendelea kupatiwa matibabu baada ya
kushambuliwa na watu wenye silaha hapo jana, shambulio ambalo
limelaaniwa vikali na pande mbalimbali.
Ferdinand
Mihigo msemaji wa Hospitali Heal Africa ya Goma amesema Mkurugenzi
huyo alipigwa risase begani, na amefanyiwa upasuaji na bado
anaendelea kupatiwa matibabu.
Mkurugenzi
huyo raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 43 mtetezi wa mazingira
aliteuliwa kwenye uadhifa huo mwaka 2008 na sasa Ubalozi wa Ubelgiji
jijini Kishasa umesema utamsafirisha kuendelea kupata matibabu jijini
Brusels.
Watu
wenye silaha walimvamia kiongozi huyo mbugani kwenye umbali wa
kilometa zaidi ya thalathini na jiji la Goma mji mkuu wa Mkoa wa Kivu
ya kaskazini ambako makundi mengi ya uasi yamekuwa yakihusika katika
kuyumbisha usalama.
Waziri
wa mambo ya nje wa ubelgiji Didier Reinders, katika Ujumbe alio
uandika kupitia mtandao wa twitter, ameahidi kuwa serikali ya
Ubelgiji itafwatilia kwa karibu hadi kuhakikisha waliohusika na
shambulio hilo wanapatikana.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire