Pages

mardi 1 avril 2014

WATU ZAIDI YA MIA TATU WATIWA NGUVUNI NCHINI KENYA WAKATI HUU USALAMA UKIIMARISHWA KATIKA JIJI LA NAIROBI


Usalama umeimarishwa katika jiji la Nairobi nchini Kenya kufuatia mfululizo wa mashambulizi ya kushtukiza yanayodaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa kundi la Al-Shabab lenye makazi yake nchini Somalia.

Jana jioni wakazi wa eneo la Eastleah jijini Nairobi wameshuhudia milipuko mitatu mfululizo ya mabomu iliyosababisha vifo vya watu sita na wengine kadhaa kujeruhiwa, kwenye eneo ambalo linakaliwa na wenyeji wengi wa Somalia.

Polisi wametangaza kuendesha msako mkali dhidi ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na ulipuaji huu wa mabomu na kuwataka raia wa Somalia walitoka kwenye kambi za wakimbizi nchini humo kurejea kwenye kambi zao.


Uchunguzi wa awali wa polisi kwenye jiji la Nairobi umeonesha kuwa tukio hilo ni lakigaidi na huenda likawa limetekelezwa na wanamgambo wa Al-Shabab ambao wameapa kutekeleza mashambulizi zaidi kama hayo kwenye maeneo ya Kenya hadi pale nchi hiyo itakapoondoa majeshi yake nchini Somalia.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...