Pages

mardi 29 avril 2014

NAVI PILLAY JIJINI JUBA WAKATI HUU MAZUNGUMZO YAKIANZA NCHINI ETHIOPIA

Navy Pillay
Mazungumzo kati ya wajumbe wa serikali ya Sudani Kusini na waasi wanaomtii makam wa rais wa zamani Riek Machar yameripotiwa kuanza tena hapo jana jijini Addis Abeba nchini Ethiopia, yakiwa na lengo la kutafuta suluhu la kisiasa na maridhiano ya kitaifa.

Hatuwa hiyo ya pili ya mazungumzo ilianza tangu mwezi Februari, na kushindwa kufikia muafaka kutokana na madai ya waasi kutaka waachiwe huru wafungwa wanne walioshukiwa kutekeleza jaribio la mapinduzi ya serikali ya rais Salva Kiir.


Mazungumzo haya yanajiri wakati huu mjumbe wa Umoja Mataifa anaye husika na haki za Binadamu Navi pillay akiwa ziarani nchini Sudani Kusini kwa ajili ya kuomba uchunguzi wa mauaji dhidi ya watu zaidi ya mia moja walipoteza maisha na ambao serikali na waasi wamekuwa wakitupiana lawama kila mmoja akimtuhumu mwingine kuhusika.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...