Pages

mercredi 9 avril 2014

BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LATIWA WASIWASI NA JOTO LA KISIASA NCHINI BURUNDI


Balozi Joy Ogwu
Rais wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Balozi kutoka nchini Nigeria Joy Ogwu amesema Wajumbe 15 wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wanatiwa wasiwasi  kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea nchini Burundi wakati huu.

Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu kikao cha baraza hilo kilichofanyika faraghani ambacho kilijadili kuhusu Burundi, Balozi Joy amesema Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anaye husika na maswala ya siasa Jeffrey Feltman ndiye ambaye aliwasilisha kwa wajumbe 15 wa baraza hilo, hali ilivyo nchini Burundi, na kusisitiza kuhusu matumizi ya nguvu kwa makundi ya vijana wa vyama vya siasa.

Wajumbe hao wamesema wote kwa kauli moja kwamba wanatiwa waziwasi na hali hiyo wakati huu nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Baraza hilo limependekeza kwa wansiasa kuketi kwenye meza ya mazungumzo bila kutenga kundi lolote na kujadili chini ya misingi ya makubaliano ya Arusha.

Burundi ambayo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hali ya joto la kisiasa imekuwa ikishuhudiwa na hata machafuko tangu kuondoka katika serikali kwa wajumbe wa chama cha Uprona.

Machafuko yameshuhudiwa March 8 iliopita jijini Bujumbura kati ya wafuasi wa chama cha upinzani cha MSD na polisi wa Usalama.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...