Umoja
wa vyama vya upinzani nchini Burundi usiokuwa na wawakilishi Bungeni,
umewatumia ujumbe marais wa Tanzania, Uganda na Afrika Kusini
kuwataka waingilia kati kuhusu hali ya kisiasa na Usalama nchini
Burundi.
Mwenyekiti
wa umoja wa vyama hivyo, Jacques Bigirimana amewaomba ma rais Jakaya
mrisho Kikwete wa Tanzania, Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na Jacob
Zuma wa Afrika Kusini kuwatuma wajumbe wao nchini humo kukutana na
pande mbalimbali ili kujuwa hali halisi inayojiri kwa sasa nchini
humo na kutowa ukweli kuhusu hali hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire