Bunge
nchini Uganda limeanza kuchunguza tuhma za wanariadha wa kike nchini
humo wanaodai walidhalalishwa kimapenzi na kocha wao.
Wabunge
nchini humo wanasema kitendo hicho ni aibu ya kitaifa na wanataka
ukweli kubainika ili hatua ichukuliwe.
Wanariadha
hao wanadai kuwa walidhalalishwa na kulazimishwa kufanya mapenzi na
kocha huyo wakati wa maandalizi ya mbo za nyika za bara Afrika
zilizofanyika nchini humo mwezi uliopita.
Inadaiwa
kuwa kocha huyo aliwaambia wanariadha hao kuwa ikiwa wanataka
kukimbia haraka na kushinda mbio hizo ni lazima wafanye naye ngono.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire