Kiongozi
mmoja wa kundi la watu wenye kuunga mkono serikali ya Urusi katika
jimbo la Slaviansk mashariki mwa Ukraine ametowa wito kwa serikali
ya Urusi na rais Vladimir Poutine kuwapa msaada katika harakati zao
wa kuipiga vita serikali yenye kuungwa mkono na Umoja wa Ulaya ya
Kiev.
Viatcheslav
Ponomarev amewatolea wito viongozi wa Urusi kuwalinda na harakati za
Ukraine ambayo inampango wa kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya
wananchi ya Donbass mashariki mwa Ukraine.
Hayo
yanajiri wakati vikosi vya serikali ya Kiev vikiwa havionekani katika
eneo hilo, licha ya kutangazwa rasmi operesheni ya kupambana na
magaidi ambao ni wanaharakati wanaounga mkono serikali ya urusi.
Viatcheslav Ponomarev amethibitisha kuwa serikali ya Kiev imewatuma
mamluki zaidi ya mia moja ili kulikomboa Jimbo la Slaviansk
lililoanguka chini ya mikono ya wanaharakati hao tangu Jumamosi
iliopita.
Tayari
Urusi imelundika majeshi yake katika maeneo ya mpaka na eneo hilo,
ambapo mfumo uliotumiwa kwa Crimea ndio unaohofiwa kutumiwa katika
majimbo hayo ya Mashariki.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire