Rais
wa Burundi Pierre Nkurunziza amefanya ziara ya kikazi nchini Somalia
hapo jana Jumanne April 22. Duru za Ikulu ya rais nchini Burundi
zimearufu kuwa ziara hiyo inalenga kudumisha uhusiano baina ya
mataifa haya mawili.
Baada ya kukutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake wa Somalia Hassan Cheukh Mahmoud, Rais
Nkurunziza amekutana na wanajeshi wa Burundi walioko nchini Somalia
na kuwapongexa kwa kazi yao nzuri wanaoifanya nchini humo ya
kurejesha amani na utulivu.
Nkurunziza
amesema vikosi vya Burundi vinaipatia sifa nzuri nchi hiyo baada ya
kuonyesha ukomavu katika shughuli za kurejesha amani na utulivu.
Baada ya ziara hiyo, rais Nkurunziza anaelekea nchini jamhuri ya Afrika ya Kati ambako atakutana na viongozi wakuu wa nchi hiyo.
Burundi ni miongoni mwa nchi zilizotuma vikosi vya kurejesha amani nchini jamhuri ya Afrika ya Kati.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire