Nchini
Tanzania wajumbe wa bunge la Katiba kutoka vyama vya upinzani
wameondoka bungeni jioni hii, baada ya kudai kuwa chama tawala
kinahujumu juhudi za upatikanaji wa Katiba mpya.
Kiongozi wa
chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba ameongoza wajumbe hao kuondoka
nje na kuwaacha wajumbe wa CCM wakiendelea kujadili rasimu hiyo
kuhusu muundo wa serikali.
Lipumba
amedai kuwa wapinzani wanabaguliwa katika mjadala huo na maoni ya
wananchi hayapewi kipaumbele.
Lipumba amesikika akiwaita wabunge wa chama tawala kuwa ni Interahamwe"Kundi la wapiganaji wa Kihutu wa Rwanda wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji ya Kimbari nchini Rwanda"
Lakini licha ya wabunge hao wa upinzani kuondoka ukumbini, Mjadala
umeendelea bungeni kuhusu muundo wa serikali ambapo chama tawala kinataka
serikali mbili na wapinzani wanataka serikali tatu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire