Pages

mercredi 30 avril 2014

WANAHARAKATI NCHINI NIGERIA WAOMBA KUPEWA TAARIFA ZA WASICHANA WALIOTEKWA NA BOKO HARAM

Jeshi la Nchini Nigeria 
Wanaharakati nchini Nigeria wamepanga kuandamana kuelekea Bungeni kudai maelezo zaidi kuhusu wapi zimefikia hatuwa za kuwaokowa wasichana waliotekwa hivi karibuni na kundi la Boko Haram na kuwataka wanajeshi kuzidisha juhudi za kuwatafuta wasichana hao.

Mratubu wa maadamano hayo Hadiza Bala Usman ameliambia shirika la habari la AFP kwamba muhimu sio mpaka liwe kundi kubwa linaloa andamana, kubwa ni kufikisha ujumbe na kuhoji wapi walipo wasichana hao waliotekwa tangu April 14 na kundi hilo la Boko haram kaskazini mwa taifa hilo.


Lengo hasa la maandamano hayo kama ilivyoelezwa ni kuvunja ukimya wa seerikali kuhusu kutekwa kwa wasichana hao ambapo majuma mawili sasa hakuna anaye juwa wapi walipo wasichana wanakadiriwa kufikia 129 huku kukiwa na taarifa za kupelekwa nchini Cameroon na Tchad kuozwa kwa viongozi wapiganaji wa Boko Haram.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...