Wanajeshi
kadhaa wa Ufaransa na wale wa Vikosi vya Umoja wa Afrika MISCA
wamejeruhiwa kwenye shambulio la risasi lililotekelezwa na mtu mmoja
mwenye silaha kwenye mji wa Bria.
Watu
walioshuhudia tukio hilo wamedai kuwa watu wenye silaha
waliwashambulia kwa risasi askari wa MISCA na wale wa Ufaransa
waliokuwa wanatoka kwenye hospitali ya Bria kutejea kwenye uwanja wa
ndege, mashambulizi yaliyodumu kwa zaidi ya dakika 30.
Shambulio
hili linatekelezwa ikiwa zimepita saa chache toka baraza la usalama
la Umoja wa Mataifa UN lipitishe azimio la kupelekwa kwa kikosi cha
wanajesho wa kulinda amani wapatao elfu 12 watakaounda MINUSCA.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire