Majengo la benki kuu BRB, Picha kwa hisani ya Gazeti la Iwacu |
Wananchi
wa Bujumbura nchini Burundi wametiwa hofu na tukio la moto
ulioshuhudiwa jana usiku katika maeneo ya benki kuu ya taifa BRB.
Moto huo uliowaka na kuwashituwa wafanyakazi wa majengo jirani na
benki hiyo na ndipo kuomba msaada wa kitengo cha polisi kinacho
husika na kuzima moto ambacho kilifika kwa wakati.
Mkurugenzi
mkuu wa Benki kuu ya taifa Ciza Jean ametuliza nyoyo na kusema moto
huo ulisababishwa na wafanyakazi wenyewe wa benki hiyo ambao walikuwa
wanatekekteza noti ambazo zimechakaa, jambo ambalo hufanyika mara
nyingi.
Tukio
hilo limewashtuwa wananchi wakaazi wa jiji la Bujumbura ambao
walihofia na kukumbuka tukio la kuteketea kwa soko kuu la jiji la
Bujumbura Januari 27 mwaka 2013
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire